Home
About Huruma
About Huruma’s work
About Tella Mande
Ways to contribute
Contact
Swehili
 

Kuhusu Huruma

Huruma ni neno la kiswahili kuwa tunajali. Linatoa kielelezo cha hali ya msukumo wa mwanzo: ya kuwa sio kumgeuzia mgongo yeye jirani alie katika mazingira magumu, kumwonyesha kuwa una jali na una huruma. Kwa wasiobahatika kuchukua jukumu kwa kusudi la kusaidia waliosetwa na familia zilizo katika uhitaji ndani ya familia.

Lilizinduliwa mwaka 2003, Huruma Women Group liliandikishwa na Halmashauri ya wilaya ya Moshi mwaka 2005 kwa hati namba MJ/MDC/No 18092005. Huruma iliinuka kutoka katika wazo anzilishi la wanawake wawili kutoka Tella Mande waliamua kuelekeza kutatua hitaji la watu katika maskani zao haswa majirani: Baada ya kuona kuwa watu wengi wameathirika na umaskini, ukosefu wa ajira na ugonjwa wa virusi vya Ukimwi, watu ambao hawajasaidiwa na serikali au wala wasamaria wema, Mary Saria alianza kuwasaidia na chakula na madawa yeye peke yake. Baadaye akampata Berther Mawenya ambaye wapo pamoja hadi leo. Pamoja na usaidizi wa wanakijiji wengine wanaojitolea na misaada ya marafiki na wafadhili Mary na Berther wameweza kukuza juhudi hii na kusaidia jamii kubwa kwa mahitaji ya lazima.

Mary Saria ana umri wa miaka 46, ni mama wa nyumbani na ameishi hapa Tella Mande kwa miaka 28. Ni mama wa watoto sita na wanne wanaishi nyumbani kwake hadi sasa hapa Tella Mande na wanasoma. Licha ya kuhudumia jamaa yake Mary hutumia muda wake na nguvu zake kutafuta watakaosaidia na kufadhili kikundi.

Berther Mawenya ana umri wa miaka 40, ameishi hapa Tella Mande kwa miaka 15. Akiwa ni mama wa nyumbani anahudumia familia ya watoto wake wanne ambao wanaishi naye hapa Tella Mande na wanasoma pia. Tangu kikundi cha Huruma kilipoanzishwa amekuwa akimsaidia Mary kutambua kusudi la kuanzisha. Kuanzia Julai 2008 amekuwa akifanya na darasa la chekechea la kikundi ambapo anafundisha hadi watoto 40.

Kikundi cha Huruma Women Group hakina kianzio wala samani yoyote ya fedha cha kwao. Tangu kianzishwa kimekuwa kikitegemea misaada toka kwa wafadhili pamoja na wanaojitolea kutoka ndani na nje ya nchi. Hadi sasa wamama hawa wanafanya kazi bila malipo yoyote, na hii ndiyo sababu waanzilishi wengine kwa masikitiko waliamua kutokuendelea na kikundi hiki, kwa sababu na wao ni wahitaji.

Kama unajisikia kufadhili kikundi hiki cha Huruma Women Group tafadhali soma maelezo ya jinsi unavyoweza kusaidia.