Home
About Huruma
About Huruma’s work
About Tella Mande
Ways to contribute
Contact
Swehili
 

Kuhusu kazi za Huruma

Kazi zote za Huruma zinaongozwa na kanuni: Kila mwanamama anao mguso wa kipekee wa huruma na uwajibikaji kwa ajili ya jirani yake na jamii yao kwa jumla. Lengo la kwanza la kikundi ni kusaidia familia masikini hapo Tella Mande. Kwa ufasaha zaidi imelenga kusaidia watoto wa jamii na uwezekano wa kupata elimu ya msingi na pia kusaidia jamii iliyopata ugonjwa au magonjwa kama Ukimwi au Saratani kupata mahitaji ya kila siku.

Kufuatana na malengo haya na kwa msaada wa ufadhili na wanaojitolea wa ndani ya Huruma:

•  wanalipa karo za shule, sare za shule na vifaa,

•  wanaendesha kituo cha chekechea hapo Tella Mande na

•  wanasaidia familia zenye magonjwa magumu na wazazi kwa chakula, madawa na usaidizi katika siku kwa siku.

 

Miradi

Ahsante kwa ufadhili wa RFA (wakala wa Tact-Aids), Executive Solution Ltd., TBL, the Kilimani Pharmacy, Machare Investment na TANAPA, Huruma wameweza kulipa karo za shule, kununua sare za shule na vitabu kwa zaidi ya watoto 50 kwa miaka michache iliyopita. Ahsante kwa Zara Tours Huruma wameweza kusajiliwa kama kikundi cha kijamii.

Mwaka 2008 Huruma waliweza kuendelea kulipa karo za shule pia kununua sare za shule kwa watoto 40. Zaidi ya hayo kikundi kwa sasa kinasaidia zaidi ya wagonjwa wa Ukimwi 20 kwa kuwatembelea, kuwasaidia vyakula, pia madawa na wakati mwingine wanawalipia pesa ya matibabu. Kuanzia mwezi Julai kikundi kinaendesha shule ya Awali katika mazingira yetu kwa watoto 40 wa umri wa mwaka mmoja hadi maika mitano.

Kikundi cha Huruma kinakusudia kuongeza idadi ya watoto wadogo na vijana na pia familia zinazopokea elimu ya kijamii na misaada ya afya. Zaidi ya hayo kinajitahidi kuanzisha kituo cha watoto na ofisi ndogo hapa Tella Mande. Kwa kutambua hili, kikundi kinajaribu kupata ufadhili na kukuza ufadhili wa ndani na nje.