About Huruma
About Huruma’s work
About Tella Mande
Ways to contribute
Contact
Swehili
 

Njia zu kuchangia

Kikundi cha Huruma Women Group ukweli kinategemea juu ya misaada ya kifedha na hali halisi ya ufadhili na kujitolea. Kwa hiyo tunazo shukrani za dhati kwa misaada, zawadi na misaada ya kujitolea kwa kazi zetu za kila siku.

•  Kama ukijisikia kutusaidia sisi kwa msaada, tunakuomba uwasiliane nasi. Tutakuwa na furaha kuongea nawe kwa kile msaada wako utakachofanya. Kwa mfano unaweza kusaidia Huruma Women Group kununua vifaa vya ofisi na shule kama meza, viti vikubwa na viti vya watoto vya kukalia, kabati au ubao.

•  Unaweza kutusaidia kwa kupata zawadi. Kuna vitu vichache ambavyo mara kwa mara vinahitajika na watoto, vijana na familia za Huruma Women Group kama vile: nguo, samani, viatu au sare na vifaa vya shule. Unaweza kuvituma moja kwa moja Huruma au unatambulisha vile unavyoweza kununua na pesa ulizonazo.

•  Jitolee pamoja nasi: Huruma Women Group inategemea halisi juu ya juhudi za wanaojitolea. Wanaojitolea toka pande zote za Dunia wanakaribishwa kusaidia Huruma Women Group kwa kufundisha watoto katika shule yao, kutembela wagonjwa wa majumbani, kusaidia wanachama wa kikundi kuchangia na kukusanya fedha na kuendelea Huruma katika mitaala ya kimaendeleo. Kama unajiskia kutaka kusaidia kwa kujitolea, tafadhali tafuta habari chini ya www.world-unite.de .