Nyumbani
Huruma Women Group – au Huruma – ni kikundi kisichokuwa cha kiserikali ni shirika la kijamii. Kusudi lake ni kutoa huduma ya kuwa jali walio katika adhari na walio katika kudharauliwa na jamii iliyosetwa na wale walioathirika na virusi vya Ukimwi hapa Tella Mande, eneo la wilaya ya Moshi, mji mdogo wa kaskazini mwa Tanzania. Kundi lililoanzishwa na kikundi cha kina mama wanaoishi katika eneo husika. Kikundi hiki ni cha kujitolea tokea uanzilishi wake.
Leo Huruma inasaidia watoto walio katika mazingira magumu wapatao 40 na familia zao, kadhalika watu 20 walioadhirika na virusi vya Ukimwi. Huduma zinazofanyika ni pamoja na kugawia chakula, nguo na huduma za kujitolea. Zaidi ya hayo kikundi kinatoa elimu na ufadhili kwa watoto na vijana ni pamoja na kulipa karo za shule, kununua sare za shule na vifaa vya shule. Mwisho kuanzia mwezi Julai 2008 wanachama wa Huruma wameanzisha na kuendesha darasa la Awali la watoto wadogo (chekechea) jirani na familia zinazosaidiwa za Tella Mande.
Huruma wana kusudi la kuboresha hali ya maisha ya familia masikini na kusababisha jamii yenye afya ya Tella Mande. Kwa kutambua lengo hili Huruma inategemea sana kujitolea. Yote yaliyopita na yaliyopo katika mradi (ikiwa ni pamoja na huu ukurasa) imewezekana kutokana na msaada wa ufadhili wa kujitolea. |